Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Khamenei vilevile, alitoa tanbihi kwa upande wa Marekani katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na, akasisitiza:
"Kauli za Wamarekani kuwa hawataruhusu Iran kufanya urutubishaji wa nyuklia ni upuuzi wa kiwango cha juu, na Jamhuri ya Kiislamu itaendeleza siasa na njia yake katika jambo hili bila kusubiri ruhusa ya mtu yeyote."
Hadhrat Ayatollah Khamenei alitaja kuwa lengo la upande wa pili kusisitiza juu ya mazungumzo ya moja kwa moja ni kuonesha taswira ya aina fulani ya kusalimu amri kwa Iran, na akasema:
"Shahidi Raisi hakuwapa nafasi hiyo. Bila shaka, katika zama zake, mazungumzo ya moja kwa moja hayakufanyika kama ilivyo sasa, na mazungumzo yaliyokuwepo yalikuwa yasiyo ya moja kwa moja, ambayo hayakufikia natija, na hivi sasa pia hatuoni uwezekano wa kupata natija, wala hatujui nini kitatokea."
Ayatollah Khamenei pia alitaja ripoti ya taasisi za kifedha za kimataifa kuhusu ongezeko la ukuaji wa uchumi wa Iran kutoka karibu asilimia sifuri mwanzoni mwa serikali ya kumi na tatu hadi karibu asilimia 5 mwishoni mwa kipindi hicho kuwa ni jambo la kujivunia, chanzo cha izza ya kitaifa na kiashirio cha maendeleo ya nchi, na akasema: "Kubeba Qur’an au picha ya Shahidi Soleimani katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa hatua nyingine alizochukua Shahidi Raisi ambazo kwa njia yake alilipa hadhi na heshima kubwa taifa la Iran.
Maoni yako